Serikali Yasifu Mchango wa ACK Katika Maendeleo ya Taifa Wakati Dayosisi Yazindua Mpango wa Mabadiliko

kasuku David 
taifa leo
   Serikali yaisifu Kanisa la Anglikana la Kenya (ACK) kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya taifa wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Miaka Mitano wa Mabadiliko ya Kijamii, Kiuchumi na Kisaikolojia wa Dayosisi ya ACK Nairobi uliofanyika Ruai, Kaunti ya Nairobi.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Rais, Profesa Kithure Kindiki, kama mgeni rasmi, pamoja na Katibu Mkuu wa Madini Elijah Mwangi, viongozi wa serikali, viongozi wa kanisa na wadau mbalimbali wa jamii.

Wakizungumza katika hafla hiyo, viongozi walipongeza ACK kwa kuunga mkono juhudi za serikali kupitia sekta za elimu, afya, uwezeshaji wa vijana, miradi ya maji na malezi ya kiroho ambayo yanaendelea kubadilisha maisha ya wananchi nchini.

Askofu wa ACK Dayosisi ya Nairobi, Jonathan Kabiru, alisema mpango huo wa miaka mitano utalenga uwezeshaji wa kijamii, kiuchumi na kisaikolojia kwa lengo la kuimarisha familia, kusaidia makundi yaliyo hatarini na kukuza maendeleo endelevu ya jamii.
Viongozi hao walisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na taasisi za kidini katika kushughulikia changamoto za kijamii zinazokabili jamii. Walibainisha kuwa licha ya Serikali kuendelea kuwekeza katika miundombinu na maendeleo ya kiuchumi, kanisa lina jukumu muhimu la kukuza maadili, mshikamano wa familia na ustawi wa kiroho.

Hafla hiyo iliwaleta pamoja viongozi wa kanisa, wazee wa kanisa, washirika wa maendeleo, viongozi wa jamii na maafisa wa serikali ambao waliahidi kuunga mkono utekelezaji wa mpango huo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Viongozi hao pia walitoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na taasisi za kidini katika kuendeleza haki, uwajibikaji, ustawi wa jamii na umoja wa kitaifa.
  Askofu wa ACK Dayosisi ya Nairobi Jonathan Kabiru ametoa wito wa kuimarishwa kwa huduma za ushauri nasaha, msaada wa kisaikolojia na malezi ya kiroho kwa wanafunzi kufuatia mkasa wa moto katika Shule ya Utumishi Girls Academy uliosababisha vifo vya wanafunzi 16.

Akizungumza Kwa hio hafula huko Ruai, Askofu Kabiru alisema visa vya hivi karibuni vya migomo na machafuko shuleni vinaashiria kuwepo kwa changamoto za kina za kihisia na afya ya akili miongoni mwa vijana. Aliwahimiza wazazi, shule, makanisa na taasisi za serikali kushirikiana katika kuwapa wanafunzi msaada na mwongozo wanaohitaji ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

Comments

Popular posts from this blog

Launch Of Raila Odinga Leadership Academy Hails New Era of Transformative Leadership

Boredo Wins Jubilant Steward of Africa Award, Highlighting Role in Sustainable Waste Management

Sugar Sector Warns of Deepening Crisis as Farmers Cite Rising Costs, Market Distortions and Policy Gaps at WFO–KENAFF Meeting