COTU Kwa Wanasiasa: Ondoeni Siasa kwa Vyama vya Wafanyakazi
COTU(Kenya)ikiongozwa na viraja wa vyama vya wafanyi Kazi Kenya imemtetea vikali Katibu Mkuu wake Francis Atwoli, ikitupilia mbali ukosoaji wa hivi karibuni kutoka kwa viongozi wa kisiasa kama “wa juu juu, wa kupotosha na unaoendeshwa na maslahi finyu ya kisiasa.”
Katika majibu makali, Kiamu Benson okwara kakita kikao na wanahabari alilisema mashambulizi yanayoongozwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua ma Fazul si tu hayana msingi bali pia ni dharau kwa historia na kujitolea kwa vuguvugu la wafanyakazi nchini Kenya.
Maafisa hao wa COTU walisema juhudi za kumchafua Atwoli zinapuuza miongo ya utetezi uliowezesha kupatikana kwa mishahara bora, mazingira mazuri ya kazi na ulinzi thabiti wa haki za wafanyakazi kwa mamilioni ya Wakenya.
“Kauli hizi ni za juu juu na zinaonyesha ukosefu wa uelewa kuhusu nafasi ya vyama vya wafanyakazi,” COTU ilisema, ikisisitiza kuwa vuguvugu la wafanyakazi si chombo cha kisiasa cha serikali yoyote bali ni taasisi huru inayotokana na mapambano ya wafanyakazi.
Shirikisho hilo pia lilikataa madai kuwa Atwoli amekaa madarakani kwa muda mrefu kupita kiasi, likieleza kuwa uongozi ndani ya vyama huchaguliwa kidemokrasia na wanachama. Pia lilitetea uhusiano wake wa kikazi na serikali, likisema ushirikiano—si mivutano—ndio huleta matokeo kwa wafanyakazi.
COTU ilitaja mafanikio ya hivi karibuni, yakiwemo ongezeko la asilimia 12 la mishahara ya jumla na ongezeko la asilimia 15 la kiwango cha chini cha mishahara kwa sekta ya kilimo, kama ushahidi kuwa mkakati wao unafanya kazi.
Chama hicho pia kilikosoa mapendekezo ya kuanzishwa kwa mwavuli mbadala wa vyama vya wafanyakazi, kikiyataja kuwa hayana msingi na yanaweza kudhoofisha umoja wa wafanyakazi.
Akiunga mkono Rev Joel chebii
alisema “Vyama vya wafanyakazi hujengwa kwa muda kupitia kujitolea na mshikamano. Haviwezi kuanzishwa mara moja kwa ajili ya maslahi ya kisiasa,” iliongeza taarifa hiyo.
Kadri mvutano unavyozidi, COTU imewataka viongozi wa kisiasa kuepuka kuingiza taasisi za wafanyakazi katika mapambano ya kisiasa, ikionya kuwa hatua hizo zinaweza kudhoofisha haki za wafanyakazi zilizopatikana kwa jasho na juhudi kubwa.
Shirikisho hilo lilithibitisha tena dhamira yake ya kuwatetea wafanyakazi na kulinda uhuru wake, likisema halitayumbishwa na kile ilichokitaja kama “siasa za kando.”
Comments
Post a Comment