Mahusiano ya Biashara kati ya Kenya na Marekani Yaongezeka Baada ya Kuongezwa kwa AGOA
Rais William Ruto amepongeza kuongezwa kwa Mpango wa African Growth and Opportunity Act (AGOA) kwa miaka mingine mitatu, akisema hatua hiyo itakuza mapato ya mauzo ya nje na kuongeza kipato cha Wakenya.
Akizungumza baada ya kukutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Christopher Landau, katika Ikulu ya Nairobi, Rais Ruto alisema kuongezwa kwa AGOA kunahakikisha bidhaa za Kenya zinaendelea kuingia soko la Marekani bila ushuru, hivyo kuwapa wazalishaji faida zaidi na kupunguza gharama za biashara.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Baraza la Mawaziri, Musalia Mudavadi, alisema kuongezwa kwa AGOA kunaleta uhakika kwa wawekezaji na wauzaji wa nje, na kuwawezesha kupanga mipango ya muda mrefu, kupanua uzalishaji na kuongeza mapato ya fedha za kigeni. Alibainisha kuwa sekta za nguo, kilimo, chai, kahawa, maua na bidhaa za viwandani zitanufaika pakubwa, jambo litakaloimarisha kipato cha wakulima, wafanyakazi wa viwandani na wafanyabiashara wadogo.
Comments
Post a Comment